Sambaza

 SHAKA SSALI ASTAAFU, KUAGWA RASMI VOICE OF AMERICA

Mtangazaji mkongwe wa Kipindi cha Straight Talk Africa kinachorushwa na Kituo cha Runinga na Redio cha Voice of America cha Washington, Marekani Shaka Ssali amestaafu rasmi majukumu yake ya uandishi wa habari.

Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa VOA, Shaka Ssali amestaafu baada ya kukitumikia kituo hicho kwa kipindi cha miaka 29, ambapo mbali na Straight Talk Africa, alikuwa pia akitangaza kipindi kingine cha Shaka: Extra Time.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba Shaka ataongoza kipindi cha mwisho cha Straight Talk Africa Jumatano ya Mei 19, 2021 ambacho kitakuwa maalum kwa ajili ya kumuaga na kuonesha heshima kwa mchango mkubwa alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa akifanya kazi.

Kipindi cha mwisho cha Shaka, kitakuwa ni maalum kwa ajili ya kuangazia safari ya uandishi wa habari ya mwanahabari huyo nguli kuanzia mwanzo alipojiunga na kituo hicho na jinsi alivyoitumia taaluma yake kuboresha demokrasia na maendeleo kwa nchi za Kiafrika.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba siku hiyo, ndipo atakapotambulishwa mrithi wa Ssali katika kipindi hicho cha Straight Talk Africa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey