KIPCHOGE Aibuka Kinara Mbio za NN Mission Marathon Nchini Uholanzi
Eliud Kipchoge, mwanariadha kutoka nchini Kenya, ameibuka mshindi katika mbio za NN Mission Marathon zilizofanyika leo Twente, Enschede nchini Uholanzi kwa kumaliza mbio hizo katika muda wa 2:04:30.
Muda alioutumia Kipchoge, ni dakika tatu zaidi tangu alipoweka rekodi ya dunia nchini Ujerumani katika Mbio za Berlin Marathon mwaka 2018 alipoweka rekodi ya muda wa 2:04:30.
Ushindi huo wa Kipchoge, umepokelewa kwa shangwe na nderemo kwa Wakenya, Afrika Mashariki na bara zima la Afrika na unatajwa kuwa hatua muhimu kwa mwanariadha huyo, kuelekea katika mashindano ya Marathon yanayotarajiwa kufanyika Agosti, mwaka huu jijini Tokyo, Japan.
Toa Maoni Yako Hapa