Sambaza

KOFFI OLOMIDE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 18

Mkongwe wa nyimbo za Rhumba kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Koffi Olomide amekutwa na hatia ya kuwateka na kuwashikilia wanawake wanne waliokuwa wanenguaji wake bila ridhaa yao katika makazi yake jijini Paris, Ufaransa.

Mahakama ya Rufaa ya Versailles ya nchini Ufaransa iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo, imetoa uamuzi huo Desemba 13, 2021 na kutengua hukumu ya mwaka 2019 iliyomkuta na hatia ya ubakaji baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza.

Kofi amekutwa na hatia ya kuwateka wanenguaji hao kati ya mwaka 2002 na 2006 ambapo kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa, amepewa adhabu ya kifungo cha miezi 18 jela, adhabu ambayo hataitumikia mpaka atakapokutwa na hatia katika makosa mengine (suspended sentence).

Pia staa huyo wa ngoma ya Papaa Ngwasuma ameamriwa kulipa faini ya kati ya dola 11,000 (shilingi milioni 25) hadi dola 36,000 (shilingi milioni 83) kwa kila mwanamke kama fidia kwa makosa aliyowatendea.

Hii si mara ya kwanza kwa Koffi mwenye umri wa miaka 65 kukumbana na mkono wa sheria, mwaka 2018 nchini Zambia aliamriwa kukamatwa baada ya kumfanyia unyanyasaji mpiga picha wake.

Mwaka 2016 alikamatwa nchini Kenya baada ya kumdhalilisha mnenguaji wake na mwaka 2012 alikutwa na hatia nchini DRC na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu baada ya kumdhalilisha prodyuza wake.

Cc; @bakarimahundu

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey