MARUFUKU KUVAA MAJAKETI YA NGOZI KOREA
Mamlaka za nchini Korea Kaskazini zimetoa onyo kali kwa wananchi wa nchi hiyo kuvaa jaketi za ngozi, kwa kile wanachokidai kuwa ni utovu wa nidhamu kwa wananchi hao kuiga vazi linalovaliwa na Rais Kim Jong Un wa nchi hiyo.
Korea Kaskazini jaketi za ngozi zimepata umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2019 baada ya Rais Kim kuonekana amevaa nguo hiyo katika kipindi cha televisheni, mwanzoni aina hiyo ya nguo ilikuwa inavaliwa na matajiri pekee lakini baada ya Rais Kim kuivaa basi wauzaji wa jaketi feki za ngozi waliingiza bidhaa hizo nchini Korea na hadi sasa wananchi wengi wanapenda kuzivaa.
Polisi wanafanya doria mtaani na sokoni ili kuwakamata wauzaji na wanunuzi wa aina hizo za nguo, Jaketi za ngozi zinaonekana kama ni alama na utambulisho wa Rais Kim kwani yeye ndiye aliyezifanya kuwa maarufu nchini humo.
Cc; @bakarimahundu