Ozil Arejeshwa Kikosini, Sasa Kuivaa Liverpool
HUENDA Mesut Ozil akachukua nafasi ya Granit Xhaka kama nahodha wa Arsenal, hii inakuja siku mbili baada ya Xhaka kutofautiana vikali na mashabiki wa Arsenal. Ozil amekuwa akikumbana na wakati mgumu klabuni hapo kwa wiki kadhaa baada ya kupigwa benchi.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa Arsenal Unai Emery, amedokeza kuwa kiungo wa kati anayezingirwa na utata Mesut Ozil huenda akakabidhiwa majukumu ya unahodha wakati Gunners watakuwa wakivaana na Liverpool katika mechi ya Kombe la Carabao mnamo Jumatano, Oktoba 30.
Hatua hii yapata siku mbili baada ya nahodha wa klabu hiyo, Granit Xhaka, kujibizana vikali na mashabiki wa Arsenal.
Xhaka aliondolewa uwanjani katika kipindi cha pili baada ya mahasidi wao wa jadi Crystal Palace kusawazisha bao lao kuwa droo ya 2-2, huku Bukayo Saka akitambulishwa mchezoni.
Mabadiliko hayo yalipokelewa kwa vifijo na nderemo kutoka kwa mashabiki wa Arsenal ambao walionyesha kutoridhishwa ni kiwango cha Xhaka.
Xhaka kwa upande wake, aliziba masikio na kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo. Tukio hilo liliamsha hasira ya mashabaiki hao huku baadhi yao wakimtaka kiungo huyo wa Uswizi kuvuliwa unahodha.
Katika kuwatuliza mashabiki, Emery alidokeza kuwa huenda Ozil akakabidhiwa jukumu la unahodha kwa kuchukuwa nafasi ya Xhaka ambaye anadai kuwa amehuzinika na pia kukata tamaa.
Muhispania huyo pia alithibitisha kuwa Ozil atakuwa miongoni mwa kikosi kitakachopambana na vijana wa Jurgen Klopp katika mechi ya kombe.
Aliulizwa mkufunzi huyo wa zamani wa Paris Saint-German, endapo Ozil atakabithiwa mikoba ya unahodha na akasema: “Itategemea huenda akawa” Ozil alikuwa amepumzishwa na Emery, huku kiungo huyo wa kati wa Ujerumani akishiriki mechi mbili pekee msimu huu.