Sambaza

Simbu: Medali ya Dunia ya Majeshi imenipa mwanga kuelekea Olimpiki 2020

 

 

MWANARIADHA nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu amesema kuwa baada ya kutwaa medali ya fedha (Silver) kwenye mashindano ya Dunia ya Majeshi yaliyo malizika hivi karibuni nchini China, anajipanga na michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika jijini Tokyo.

Simbu ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi za Global Group, zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na Kapteni wa timu ya Taifa ya Jeshi upande wa riadha ambayo ilikwenda kushiriki mashindano hayo ya Dunia ya Majeshi, Mohamed Kasui.

Katika stori za hapa na pale zilizokuwa zikiendelea ndani ya +255 Global Radio, Simbu alisema kuwa “Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata hii medali ya fedha, kwenye haya mashindano naweza kusema kuwa yalikuwa na changamoto zake kama ambavyo mnajua wanariadha tulikimbia wengi na kila mmoja alikuwa anataka ushindi.

“Pili nitoe shukrani zangu kwa viongozi wangu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwani wao ndio sababu kubwa ya mimi kuwa hapa nilipo na jina langu kuendelea kuwika Kitaifa na Kimataifa.

Akizungumzia mikakati aliyonayo katika kuelekea mashindano ya Olimpiki 2020, Simbu alisema atakapo rudi jijini Arusha ambako ndiko kwenye makazi yake, atahakikisha ana anza mazoezi ya nguvu kujiweka tayari na vita hiyo ili aweze kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.

“Kuelekea Olimpiki 2020 sio mbali, ni wakati wakuanza maandalizi ya mapema ili Tanzania itakapo shiriki tuibuke na medali ya dhahabu,” alisema Simbu.

 

Mbali na mashindano hayo ya Dunia ya Majeshi, mwezi uliopita Simbu alikimbia mashindano ya Dunia yaliyofanyika jijini Doha nchini Qatar na kufanikiwa kukamata nafasi ya 16 dhidi ya Mataifa pinzani.

Nchi ya kwanza iliyoongoza kwakuzoa medali nyingi katika mashindano hayo ni Marekani ambao walibeba dhahabu 14, fedha 11 nashaba 4 wakifuatiwa na majirani Kenya ambao walibeba dhahabu tano, fedha mbili na shaba nne wakati Jamaika wao wakishika namba tatu kwa wingi wa medali ambapo dhahabu walichukuwa tatu, fedha tano na shaba nne.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey